Editors Choice

3/recent/post-list

Forbes: JAY-Z na Rihanna wanamuziki mabilionea, Kanye West nje, Elon Musk namba mbili

 JAY-Z na Rihanna wameendelea kui-run town.

Kwa mujibu wa Forbes, wanamuziki hao ni miongoni mwa watu matajiri zaidi duniani. Kwenye list ya watu wenye utajiri mkubwa zaidi iliyotolewa mwaka huu, kuna mabilionea  2,640 wakiwemo Jeff Bezos na Bill Gates.



Shawn “JAY-Z” Carter yupo namba 1217 akiwa na utajiri wa dola bilioni 2.5.

JAY-Z ambaye 2019 alitajwa kuwa rapa wa kwanza bilionea, utajiri wake umetajwa kuchochewa na Roc Nation, Armand de Brignac pamoja na mauzo ya D’USSE. JAY-Z kwenye nafasi yake yupo sambamba na Oprah Winfrey.

Rihanna ameingia kwenye nafasi ya 2020 akiwa na utajiri wa dola bilioni 1.4 za marekani. Rihanna mwenye miaka 35, vyanzo vyake vya mapato makubwa ni biashara ya Fenty Beauty pamoja na Savage X Fenty.

Baada ya kuwa na mwaka mgumu 2022, ilithibitishwa kuwa mkataba wa Kanye West kuuza viatu vya adidas kwa nembo ya YEEZY ulisitishwa, kusitishwa kwa mkataba huo, kumemfanya Kanye West kutolewa kwenye list ya mabilionea. Kanye West alitajwa namba 1513 mwaka 2022 akiwa na utajiri wa dola bilioni 2 ambao umeporomoka mpaka dola milioni 398. Mke wake wa zamani, Kim Kardashian amebakia kuwa bilionea kwenye nafasi ya 2259 akiwa na dola bilioni 1.2. Lebron James na Tyler Perry wamekutana kwenye nafasi ya 2540.

Jumla ya utajiri wa mabilionea wote duniani ni dola trilioni 12.2. Elon Musk ameshuka mpaka nafasi ya pili baada ya ununuzi wa twitter kuzigharimu hisa zake Tesla. . CEO wa LVMH Bernard Arnault ndiye mtu tajiri zaidi duniani akiwa na utajiri wa dola bilioni 211.

Post a Comment

0 Comments